Eliza Dushku
Eliza Patricia Dushku (amezaliwa tar. 30 Desemba 1980) ni mwigizaji wa tamthilia za TV na filamu kutoka nchini Marekani. Ameonekana katika filamu nyingi tu za Hollywood, filamu hizo ni True Lies, The New Guy, Bring It On, na Wrong Turn.
Eliza Dushku | |
---|---|
Eliza kwenye Tribeca Film Festival mnamo 2012 | |
Amezaliwa | Eliza Patricia Dushku 30 Desemba 1980 Massachusetts |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1992–hadi leo |
Ndoa | Rick Fox (2009-hadi leo) |
Vilevile ni anafahamika zaidi kwa kushiriki katika mfululizo wa vipindi vya televisheni, Buffy the Vampire Slayer na Angel as Faith. Pia alikuwa mwusika mkuu katika katika mfululizo wa kipindi cha tevisheni, maarufu kama Tru Calling.
Wasifu
haririMaisha ya awali
haririDushku alizaliwa mjini Watertown, Massachusetts. Baba wa Dushku alikuwa Mwalbania-Mwamerika na mamake alikuwa Mdenmark asilia. Alikulia katika dhehebu la Mormon, ambalo mamake ndilo alilokuwa anaamini, lakini yeye hakujiweka karibu sana na dhehebu hilo. Ana ndugu watatu wa kiume, Aaron, Benjamin (amezaliwa 5 Februari 1976), na Nathan (amezaliwa 8 Juni 1977, mjini Boston, Massachusetts), wa mwisho wake nae vilevile mwigizaji na mwanamitindo. Wazazi wake na Dushku walitarikiana tangu Dushku akiwa yungali bado mchanga.
Maisha binafsi
haririDushku kwa sasa anaishi mjini Los Angeles, California.
Filamu alizoigiza
hariri- That Night (1992) - Alice Bloom
- This Boy's Life (1993) - Pearl
- Fishing With George (1994)
- True Lies (1994) - Dana Tasker
- Bye Bye Love (1995) - Emma Carlson
- Journey (1995, TV) - Cat
- Race the Sun (1996) - Cindy Johnson
- Bring It On (2000) - Missy Pantone
- Jay and Silent Bob Strike Back (2001) - Sissy
- Soul Survivors (2001) - Annabel
- The New Guy (2002) - Danielle
- City by the Sea (2002) - Gina
- Wrong Turn (2003) - Jessie Burlingame
- Punk'd (2003) - Herself
- The Kiss (2003) - Megan
- The Last Supper (2006) - Waitress
- Yakuza (2006, Video Game) - Yumi Sawamura (voice)
- On Broadway (2007) - Lena Wilson
- Nobel Son (2007) - Sharon "City" Hall
- Open Graves (2007) - Erica
- The Alphabet Killer (2007) - Megan Paige
- Bottle Shock (2008)
- Sex and Breakfast (2008) - Renee
Vipindi vya televisheni
hariri- Buffy the Vampire Slayer (1998-1999, 2000, 2003 recurring) - Faith Lehane (sinema 20)
- Angel (2000, 2003 guest appearances) - Faith Lehane (sinema 6)
- King of the Hill (2002) - Jordan (voice) in episode 'Get Your Freak Off'
- Tru Calling (2003-2005) - Tru Davies (sinema 27 )
- Reading Rainbow (2005 guest appearance) - Mwandishi wa sinema 'Unique Monique'
- That '70s Show (2005 guest appearance) - Sarah
- Nurses (2007) - Eve Morrow (Pilot)
- Ugly Betty (2007 mgeni mwalikwa) - halijulikani
- Dollhouse (2008) - Echo
Marejeo
hariri- http://www.truefan-eliza.com/judy.html Ilihifadhiwa 18 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.maximonline.com/articles/index.aspx?a_id=4046&src=fc Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- http://movies.about.com/library/weekly/aa050202b.htm Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- http://moviesblog.mtv.com/2007/05/15/eliza-dushku-joins-the-force-for-alphabet-killer/ Ilihifadhiwa 1 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.eonline.com/gossip/kristin/detail/index.jsp?uuid=972f7d73-e0a2-43ea-abad-0abf6afba1f3