Eneo bunge la Embakasi
(Elekezwa kutoka Eneo Bunge la Embakasi)
Eneo Bunge la Embakasi lilikuwa jimbo la uchaguzi nchini Kenya, moja kati ya maeneo bunge ya Mkoa wa Nairobi. Lilijumuisha vitongoji vya mashariki na kusini mashariki vya Nairobi. Ikiwa na wapiga kura waliosajiliwa takribani 164,227, lilikuwa ndilo eneo bunge lenye wapiga kura wengi sana nchini Kenya. Lilikuwa na mipaka sawia na tarafa ya Embakasi. Eneo lote la eneo bunge hili lilikuwa katika eneo la Baraza la Jiji la Nairobi. Lilikuwa na ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 208.
Kwa sasa limegawanywa katika maeneo bunge mapya.
Wabunge
haririMwaka wa Uchaguzi | Mbunge [1] | Chama | Vidokezo |
---|---|---|---|
1963 | John David Kali | KANU | |
1966 | B. Mwangi Karungaru | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1969 | B. Mwangi Karungaru | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1974 | Godfrey Muhuri Muchiri | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1976 | Ezra H. Njoka | KANU | Uchaguzi mdogo, Mfumo wa chama kimoja |
1979 | Ezra H. Njoka | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1983 | Godfrey Muhuri Muchiri | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1988 | David Mwenje | KANU | Mfumo wa chama kimoja |
1992 | Henry Ruhiu | FORD-Asili | |
1997 | David Mwenje | Democratic Party (DP) | |
2002 | David Mwenje | NARC | |
2007 | Mugabe Were | ODM | Aliuliwa Januari 2008 |
2008 | Ferdinand Waititu | PNU | Uchaguzi mdogo (10 Juni) [2] |
Taarafa na wadi
haririTaarafa | |
Taarafa | Idadi ya Watu* |
---|---|
Dandora | 154,157 |
Embakasi | 32,027 |
Kariobangi South | 24,528 |
Kayole | 137,866 |
Mukuru kwa Njenga | 86,697 |
Njiru | 25,251 |
Ruai | 17,531 |
Umoja | 137,866 |
Jumla | 434,157 |
*Sensa ya 1999 [3]. |
Wadi | |
Wadi | Wapiga kura waliosajiliwa |
---|---|
Dandora A | 17,223 |
Dandora B | 21,735 |
Embakasi / Mihang'o | 13,322 |
Kariobangi South | 8,589 |
Kayole | 27,506 |
Komarock | 9,413 |
Mukuru | 22,060 |
Njiru / Mwiki | 7,705 |
Ruai | 5,944 |
Savanna | 10,149 |
Umoja | 20,581 |
Jumla | 164,227 |
Septemba 2005 | [4] |
Marejeo
hariri- ↑ Center for Multiparty Democracy: Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- ↑ Daily Nation, 12 Juni 2008: Kibaki congratulates by-election winners Archived 15 Juni 2008 at the Wayback Machine.
- ↑ information.go.ke: CDF allocation by sector and location (2003-6)
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency
Viungo vya nje
hariri- Ramani ya Eneo Bunge la Embakasi
- Uchaguzikenya.com - Eneo Bunge la Embakasi Archived 17 Julai 2011 at the Wayback Machine.