Eneo bunge la Embakasi

Eneo Bunge la Embakasi lilikuwa jimbo la uchaguzi nchini Kenya, moja kati ya maeneo bunge ya Mkoa wa Nairobi. Lilijumuisha vitongoji vya mashariki na kusini mashariki vya Nairobi. Ikiwa na wapiga kura waliosajiliwa takribani 164,227, lilikuwa ndilo eneo bunge lenye wapiga kura wengi sana nchini Kenya. Lilikuwa na mipaka sawia na tarafa ya Embakasi. Eneo lote la eneo bunge hili lilikuwa katika eneo la Baraza la Jiji la Nairobi. Lilikuwa na ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 208.

Kwa sasa limegawanywa katika maeneo bunge mapya.

Wabunge

hariri
Mwaka wa Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1963 John David Kali KANU
1966 B. Mwangi Karungaru KANU Mfumo wa chama kimoja
1969 B. Mwangi Karungaru KANU Mfumo wa chama kimoja
1974 Godfrey Muhuri Muchiri KANU Mfumo wa chama kimoja
1976 Ezra H. Njoka KANU Uchaguzi mdogo, Mfumo wa chama kimoja
1979 Ezra H. Njoka KANU Mfumo wa chama kimoja
1983 Godfrey Muhuri Muchiri KANU Mfumo wa chama kimoja
1988 David Mwenje KANU Mfumo wa chama kimoja
1992 Henry Ruhiu FORD-Asili
1997 David Mwenje Democratic Party (DP)
2002 David Mwenje NARC
2007 Mugabe Were ODM Aliuliwa Januari 2008
2008 Ferdinand Waititu PNU Uchaguzi mdogo (10 Juni) [2]

Taarafa na wadi

hariri
Taarafa
Taarafa Idadi ya Watu*
Dandora 154,157
Embakasi 32,027
Kariobangi South 24,528
Kayole 137,866
Mukuru kwa Njenga 86,697
Njiru 25,251
Ruai 17,531
Umoja 137,866
Jumla 434,157
*Sensa ya 1999 [3].
Wadi
Wadi Wapiga kura waliosajiliwa
Dandora A 17,223
Dandora B 21,735
Embakasi / Mihang'o 13,322
Kariobangi South 8,589
Kayole 27,506
Komarock 9,413
Mukuru 22,060
Njiru / Mwiki 7,705
Ruai 5,944
Savanna 10,149
Umoja 20,581
Jumla 164,227
Septemba 2005 | [4]

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri