Ferreol wa Uzes (Narbonne, 5304 Januari 581) alikuwa askofu wa Uzès (553-581; labda wa Nîmes pia) nchini Ufaransa.

Alijitahidi kuvuta Wayahudi katika Ukristo, jambo lililomfanya atazamwe kwa kijicho na hatimaye afukuzwe na mfalme Kildebati I mwaka 555 hadi 558[1]. Baada ya hiyo miaka mitatu alitambuliwa kuwa kweli mtu wa Mungu akarudishwa jimboni akipokewa kwa furaha kubwa[2].

Pia alianzisha monasteri wa Kibenedikto na kuipatia kanuni iliyotunzwa hadi leo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, sawa na dada yake, Tarsisia wa Rodez, mkaapweke.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Januari[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Vita Ferreoli, apud Marcus Antonius Dominicy, Ausberti Familia Rediviva, published in Paris, 1648 (Jewish Encyclopedia)
  2. Martyrologium Romanum
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.