Filipo na Herme (walifariki Edirne, leo nchini Uturuki, 303 hivi) walikuwa askofu wa Marmara Ereğli na shemasi wake waliofia dini ya Ukristo katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano wa Dola la Roma.

Dhuluma hiyo ilipoanza, askofu Filipo aliagizwa kufunga kanisa na kuonyesha vyombo vya ibada na vitabu vyote vilivyokuwemo; kwa kuwa alimjibu gavana Yustino kwamba haikuwa halali wala mwenyewe kutoa vitu hivyo wala yeye kujitwalia, baada ya kufungwa na kuteswa, alichomwa moto pamoja na shemasi Herme.[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Oktoba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.