Open main menu
Jumba la Meya wa Fabriano, lililojengwa wakati wa utoto wa Fransisko Venimbeni.

Fransisko Venimbeni wa Fabriano (2 Septemba 1251 - 22 Aprili 1322) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Fabriano (Italia).

Anaheshimiwa kama mwenye heri.

MaishaEdit

Kisha kumaliza masomo yake ya sayansi za jamii na falsafa, alijiunga na Wafransisko mwaka 1267, akajikita katika masomo ya teolojia, uandishi na utume katika mji wake asili na maeneo ya kandokando.

Alikuwa wa kwanza kuipatia konventi ya shirika lake maktaba kubwa.

MaandishiEdit

Maandishi yake ("Chronica Marchiæ et Fabriani", "De veritate et excellentiâ Indulgentiæ S. Mariæ de Portiuncula", "Opusculum de serie et gestis Ministrorum Generalium", "Ars Prædicantium", mbali na "Hotuba" na vitabu vingine) yamepotea karibu yote.

Heshima baada ya kifoEdit

Mapema alianza kuheshimiwa kama mwenye heri. Hatimaye Papa Pius VI alithibitisha uhalali wa heshima hiyo mwaka 1775.

Viungo vya njeEdit