Frediani
Frediani (pia: Frigianu; Eire ya Kaskazini[1], karne ya 6; Lucca, Italia wa leo, 18 Machi 588 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 560 hivi[2].
Kabla ya hapo alikuwa mmonaki tena mkaapweke karibu na Lucca. Waumini walikwenda kumtafuta upwekeni awe askofu wao. Alikusanya waklero waishi monasterini.
Alifaulu kuleta wavamizi Walombardi katika Kanisa Katoliki lakini pia kuchimba mfereji wa kuelekeza mto Serchio baharini ili kugeuza madimbwi kuwa mashamba[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Online, Catholic. "St. Frediano - Saints & Angels". Catholic Online (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-09-07.
- ↑ "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Lucca". www.newadvent.org. Iliwekwa mnamo 2020-09-07.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/78150
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |