Gabriel Martinelli
Gabriel Teodoro Martinelli Silva (anajulikana kama Gabriel Martinelli, alizaliwa 18 Juni 2001 [1]) ni mchezaji wa soka wa nchini Brazil ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Ligi kuu Uingereza Arsenal FC na timu ya taifa ya Brazil.
Martinelli alizaliwa na kukulia huko Guarulhos, alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya wakubwa akiichezea timu ya Ituano na akasajiliwa na Arsenal Julai 2019, akiwa na umri wa miaka 18. Alishinda Kombe la FA katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Arsenal.
Kazi ya mpira
haririItuano
haririMartinelli alianza kazi mnamo 2010, akichezea timu ya Corinthians' futsal team. Baada ya kufanya vyema katika nyanja za soka, alihamia Ituano mwaka 2015[2] , baada ya kufanya majaribio katika klabu za Manchester United na Barcelona. Martinelli alifunga bao lake la kwanza akiwa mchezaji wa kulipwa mnamo tarehe 8 Septemba 2018, akifunga la goli la pili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Taboão da Serra, katika mashindano ua Copa Paulista ya mwaka huo.[3]
Arsenal
haririMartinelli aliripotiwa kuhitajika na baadhi ya vilabu kadhaa lakini alisaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal mnamo tarehe 2 Julai 2019, kwa ada iliyoripotiwa ya paundi milioni 6 ($ 46.9 milioni). Martinelli alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza, tarehe 11 Agosti 2019 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United, akiingia dakika ya 84 akichukua nafasi ya Henrikh Mkhitaryan. Mnamo tarehe 5 Agosti 2022, Martinelli aliifungia Arsenal katika ushindi wao wa 2-0 ugenini dhidi ya Crystal Palace, na kuwa Mbrazil wa kwanza kufunga bao la ufunguzi wa msimu katika kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza, Mnamo tarehe 3 Februari 2023, Martinelli alisaini mkataba mpya wa muda mrefu na kilabu. Mkataba huo ulikuwa wa miaka minne na nusu, ukimunganisha na klabu hiyo hadi 2027.[4][5]
Marejeo
hariri- ↑ "Gabriel Martinelli". Arsenal F.C. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ele fez mais de 200 gols na base do Corinthians, foi para o Ituano e agora é testado no United" [He scored more than 200 goals at Corinthians' youth setup, went to Ituano and now is trialled at United] (kwa Kireno (Brazili)). ESPN Brasil. 28 Julai 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-24. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Quem é Martinelli? Artilheiro da Copinha trocou o Corinthians pelo Ituano e é monitorado pelo Barça" [Who is Martinelli? Copinha goalscorer changed Corinthians for Ituano and is targeted by Barça] (kwa Kireno (Brazili)). Globo Esporte. 11 Januari 2019. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Gabriel Martinelli signs new long-term contract". Arsenal. 3 Februari 2023. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Gabriel Martinelli: Arsenal forward signs new contract with Premier League leaders until 2027". Sky Sports News. 3 Februari 2023. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gabriel Martinelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |