Gabriel Mmole
Gabriel Mmole (1939 - 15 Mei 2019) alikuwa askofu Mkatoliki nchini Tanzania.
Maisha
haririGabriel alizaliwa Mbwinji, wilaya ya Masasi, mkoa wa Mtwara.
Baada ya masomo yake ya falsafa na tauhidi, alipewa daraja takatifu ya upadre huko Ndanda-Mtwara mwaka 1971.
Baada ya upadrisho, alifanya kazi za kichungaji katika parokia kadhaa kabla ya kwenda masomoni nchini Uganda. Kisha kurudi toka masomoni, alifanywa gombera wa seminari ndogo ya Namupa iliyopo jimbo la Lindi tangu mwaka 1974 mpaka 1988.
Alitangazwa askofu wa Mtwara Machi 25 1988 na kuwekwa wakfu Mei 25 1988 na kardinali Laurean Rugambwa. Madhehebu ya kuwekwa wakfu yalifanyika katika kanisa kuu la Mtwara na kuhudhuriwa na maaskofu, mapadre, watawa na maelfu ya walei na watu wengine wenye mapenzi mema.
Tangu mwaka huo hadi tarehe 15 Oktoba 2015 alikuwa askofu wa Jimbo la Mtwara.
Chini ya utawala wake, zilianzishwa parokia za Shangani West, Namombwe, Mahurunga na Mt. Benedikto, Newala. Ameanzisha pia sekondari ya masista, Mtwara na chuo kikuu cha STEMMUCO.
Askofu Mmole alikuwa mwandishi ambaye ameandika vitabu vya Uchumba si Ndoa, Ndoa yenye Doa, Nyinyi ni Chumvi ya Dunia na Mwanga wa Ulimwengu.
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |