Gaudensi wa Brescia (alifariki 410 BK) anakumbukwa kama askofu wa Brescia (Italia Kaskazini) kuanzia mwaka 387 hadi kifo chake.

Mt. Gaudensi alivyochorwa.

Mhubiri maarufu, rafiki wa Yohane Krisostomo, aliwekwa wakfu na Ambrosi wa Milano, ingawa kwanza alitaka kukataa cheo cha uaskofu[1] akachangia juhudi za kukamilisha uenezi wa Ukristo kote Italia baada ya Kaisari Theodosi I kuufanya dini rasmi ya Dola la Roma.

Kati ya maaskofu wa wakati wake aling'aa kwa ubora wa mafundisho na maadili yake. Alielimisha watu wake kwa mahubiri na kwa maandishi.

Vimetufikia vitabu vyake ishirini na viwili[1] na hotuba kumi[2]. Aliandika pia nyaraka nyingi za kichungaji.

Alijenga basilika aliloliita Mkusanyiko wa Watakatifu [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Oktoba[4].

Tazama pia

Tanbihi

  1. 1.0 1.1 CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: St. Gaudentius
  2. http://saints.sqpn.com/saintg25.htm Ilihifadhiwa 20 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine. Patron Saints Index: Saint Gaudentius
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-23. Iliwekwa mnamo 2020-10-24.
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.