Gesi ya machozi ni silaha ya kikemia inayosababisha maumivu kwenye macho na pia kwenye njia ya pumzi. Inatumiwa kama silaha isiyoua lakini kwa viwango vikubwa inaweza kuleta madhara makubwa zaidi, hadi kusababisha kifo.

Gesi ya machozi ikitumika nchini Ufaransa mnamo 2007
Mlipuko wa gesi ya machozi ulilipuka juu ya kuruka huko Ugiriki

Kwenye jicho inakera neva za tezi za machozi zinazoanza kutoa machozi.

Kuna dawa mbalimbali zinazotumika kwa kutengeneza gesi ya machozi,

Gesi hiyo hutumiwa kwa kawaida na polisi kwa kutawanya umati mkubwa wa watu, kuvunja maandamano au kutuliza ghasia[1].

Hairuhusiwi kuitumia vitani maana matumizi ya gesi dhidi ya wanajeshi hukataliwa na mikataba ya kimataifa, baada ya vita ya gesi sumu wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Hatua za kujikinga hariri

Njia bora zaidi ya kujikinga ni kuvaa kichuja hewa usoni. Pale ambapo hakipatikani, miwani ya kuogelea (goggles) inafaa kukinga macho, pamoja na kitambaa kinyevu kinachoshikwa mbele ya mdomo na pua kama kinga ya njia za pumzi. [2]

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gesi ya machozi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.