Gladys Akpa

mchezaji wa mpira wa miguu

Gladys Akpa (alizaliwa 1 Januari 1986) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa nchini Nigeria ambaye anacheza kama beki wa klabu ya wanawake ya Sunshine Queens na timu ya taifa ya wanawake nchini Nigeria. Alikuwa sehemu ya timu katika mashindano ya wanawake ya Afrika mwaka 2010 na michuano ya wanawake ya Afrika mwaka 2012. Alicheza katika mechi ya Nigeria dhidi ya Mali ya 20 Novemba 2016, Nigeria dhidi ya Ghana mnamo 23 Novemba 2016 Mchezo wa Nigeria dhidi ya Kenya 26 Novemba 2016, Nigeria dhidi ya Afrika Kusini ya 29 Novemba 2016 na Nigeria dhidi ya Kamerun 3 Desemba 2016. [1][2]

Gladys Akpa
Amezaliwa 1 Januari 1986
Nigeria
Nchi Nigeria
Kazi yake Mwanasoka

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gladys Akpa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.