Hori Kuu ya Australia

(Elekezwa kutoka Great Australian Bight)

Hori Kuu ya Australia ni hori kubwa iliyopo upande wa kusini wa Bara la Australia.

Ramani ya Australia, inayoonyesha mipaka tofauti za Hori Kuu ya Australia: kijani kadiri ya taasisi ya Australia, nyekundu kadiri ya Shirika la Kimataifa la Hidrografia.
Hori kuu ya Australia kusini mwa Nullarbor. Picha ya NASA.

Kuna namna tofauti za kuangalia sehemu hii ya bahari kati ya wataalamu wa Australia na wataalamu wa kimataifa.

Taasisi ya Hidrografia ya Autralia inafafanulia hivi:

Mipaka yake ni Rasi Pasley katika Australia ya Magharibi na Rasi Carnot katika Australia Kusini zilizo na umbali wa km 1,160.[1] Taasisi hii inatazama Hori Kuu ya Australia kuwa sehemu ya Bahari ya Kusini.

Shirika la Kimataifa la Hidrografia linaangalia eneo kubwa zaidi likitazama mstari baina ya Rasi ya Magharibi ya Howe (35°08′S 117°37′E) hadi Rasi ya Kusini Magharibi ya Kisiwa cha Tasmania kuwa mpaka wa kusini. Kwao hori ni sehemu ya Bahari Hindi.

Hakuna miji mikubwa kwenye pwani hiyo. Tabianchi ya pwani ni yabisi, sehemu kubwa ni tambarare inayoitwa "Nullarbor" inayomaanisha "pasipo miti",

Miamba mikali ya pwani la Hori Kuu.

Marejeo hariri

  1. Great Australian Bight. Encyclopaedia Britannica. Iliwekwa mnamo 29 September 2011.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: