Gregori Palamas (kwa Kigiriki Γρηγόριος Παλαμάς) (Konstantinopoli, 1296Thesalonike 1359) alikuwa mmonaki kwenye Mlima Athos (leo nchini Ugiriki) akawa Askofu mkuu wa Thesalonike na mwanateolojia maarufu hasa kwa kutetea Hesukia dhidi ya Barlaam wa Seminara.

Baadhi ya maandishi yake yamekusanywa katika Filokalia.

Anaheshimiwa kama mtakatifu katika Makanisa ya Kiorthodoksi, lakini pia katika baadhi ya Makanisa Katoliki ya Mashariki yanayofuata liturujia ya Ugiriki[1]

Makanisa hayo yanamheshimu hasa katika Dominika ya pili ya Kwaresima kuu (Dominika ya Gregori Palamas) pamoja na kumwadhimisha katika sikukuu yake tarehe 14 Novemba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Papa Yohane Paulo II alimtaja mara kadhaa kama mtakatifu: Homily at Ephesus, 30 November 1979, General Audience, 14 November 1990, General Audience, 12 November 1997, General Audience, 19 November 1997, Jubilee of Scientists

Maandishi yake yanapopatikana

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.