Guido van Rossum
Guido van Rossum, (alizaliwa 31 Januari, 1956) ni mtayarishajiwa programu (programa) nchini Uholanzi anayejulikana zaidi kama mwanzilishi wa lugha ya programu ya Python, ambaye alikuwa na wadhifa wa benevolent dictator for life (BDFL) hadi alipojiuzulu kutoka wadhifa huo mnamo Julai 2018.[1][2] Alibaki kuwa mshiriki wa Baraza la Uendeshaji la Python hadi mwaka 2019, na akajiondoa kwenye uteuzi wa uchaguzi wa mwaka 2020.[3]
Maisha na Elimu
haririVan Rossum alizaliwa na kukulia nchini Uholanzi, ambapo alipata shahada ya uzamili katika hisabati na sayansi ya kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam mnamo 1982. Ana kaka yake, Just van Rossum, ambaye ni mbunifu wa aina (type designer) na mpanga programu ambaye alibuni chapa iliyotumiwa kwenye nembo ya Python.[4]
Van Rossum anaishi Belmont, California, na mkewe Kim Knapp,[5] na mtoto wao wa kiume.[6][7][8] Kulingana na ukurasa wake wa nyumbani na mikusanyiko ya majina ya Kiholanzi, " van " katika jina lake lina herufi kubwa anapotajwa kwa jina la ukoo pekee, lakini sio wakati wa kutumia jina lake la kwanza na la mwisho kwa pamoja.[9]
Marejeo
hariri- ↑ "Benevolent dictator for life", Linux Format, 1 February 2005. Retrieved on 2022-04-05. Archived from the original on 2006-10-01.
- ↑ "Transfer of power".
- ↑ "Steering Council nomination: Guido van Rossum (2020 term)".
- ↑ Thomas, Jockin (Mei 28, 2016). "Learning Python Makes You A Better Designer: An Interview with Just van Rossum". Medium. Iliwekwa mnamo Oktoba 25, 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Manheimer, Ken (6 Juni 2000). "(Python-Dev) Guido and Kim married". Python-Dev -- Python core developers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2010.
- ↑ "Guido van Rossum - Brief Bio". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2014.
- ↑ "(Mailman-Announce) forwarded message from Guido van Rossum". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Mei 2008.
Oh, and to top it all off, I'm going on vacation. I'm getting married and will be relaxing on my honeymoon.
- ↑ van Rossum, Guido. "What's New in Python?" (PDF). "Not your usual list of new features". Stanford CSL Colloquium, 29 October 2003; BayPiggies, 13 November 2003. Elemental Security. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 27 Juni 2010.
- ↑ van Rossum, Guido. "Guido's Personal Home Page". Iliwekwa mnamo 2 Feb 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Guido van Rossum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |