Hali Ngumu ni jina la wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original katika miaka ya 1980 mwishoni na 1990 mwanzoni. Ni kati ya nyimbo zilizotamba sana katika miaka hiyo.

"Hali Ngumu"
Wimbo wa Marquis Original
Umetolewa 1989-1990
Umerekodiwa 1989-1990
Aina ya wimbo Muziki wa dansi
Lugha Kiswahili
Urefu 7:38

Mashairi yake anazungumzia mkewe ambaye analalamikia maisha magumu na kutoa siri za ndani, yaani, mambo ya mume na mkewe. Hivyo basi anamsihi wakumbuke walipotoka na asiwasikilize hao vijino pembe.

Hivyo basi abadili mwenendo wake na atakachopata atamtimizia, zaidi ya hapo hawezi kwani maisha yake yatakwenda kombo.

Wahusika hariri

Tazama pia hariri

Viungo vya Nje hariri