Mashoga
Mashoga ni jina la wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original katika miaka ya 1980 mwishoni na ya 1990 mwanzoni. Ni moja kati ya nyimbo zilizotamba sana miaka hiyo.
"Mashoga" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Marquis Original | ||
Umetolewa | 1989-1990 | |
Umerekodiwa | 1989 | |
Aina ya wimbo | Muziki wa dansi | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 6:52 |
Mashairi yake anazungumzia mashoga na fitina za ndoa. Analalamika wanamchunguza yeye wakati yeye hawachunguzi. Wanajifanya kwake wazuri huku wanamteta. Kila apitapo wanamtazama kavaa nini, anaomba wamuache yeye ni wake wametoka mbali.
Humu walitumia sana mtindo wa "Sendema" mtindo maarufu sana kwa bendi hii. Kama ilivyo kawaida wa muziki wa dansi, sehemu kubwa inapiga vyombo tupu kama tumbuizo kwa wasikilizaji. Midomo ya bata (tarumbeta) zimepigwa vilivyo katika wimbo huu - kwa umahiri wa hali ya juu.
Wahusika
hariri- Mpiga Solo - Dekula Kahanga
- Mpiga Solo la 2 - Steven Kaingilila
- Mpiga rythm - Mulenga Kalonji
- Mpiga besi - Banza Mchafu
- Mpiga Dramz - Mharami Seseme
- Mpiga Congas - Seif Said
- Mpiga Sax - Berry Kankonde na Mukuna Roy
- Mpiga Tarumbeta - Kaumba Kalemba
- Mtunzi wa wimbo - Ngoie Mubenga
- Waimbaji: Issa Nundu, Parash Mukumbule, Mutombo Audax na Tshimanga Assosa.