Halloween
Halloween ni sherehe inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Oktoba ili kuwakumbuka wafu, watakatifu na waliouawa kwa sababu ya imani yao.
Maadhimisho hayo huwa na kuvalia nguo ya kuogofya, kutaniana, kutembelea mahala kuliko makaburi na kusikokaliwa na watu. Watu pia husimuliana hadithi za kuogofya zitakazowafanya wengine kutishika.
Wakristo husherehekea Halloween kwa kuwasha mishumaa na kuenda kanisani wanakoombea wafu wao. Wengine hujifunga kula nyama ili kuwakumbuka walio wafu.
Historia ya Halloween
haririMaadhimisho ya Halloween yalianza kutokana na sherehe za mavuno za Wakelti, hasa ile iliyoitwa Samhain. Watu wengine wanaamini kuwa Halloween ilianza kama sherehe za Kikristo (kesha la sikukuu ya Watakatifu wote). Sherehe imepata sura yake ya kutisha na ya kibiashara katika karne ya 20 nchini Marekani na kutoka huko imeenezwa katika nchi nyingi duniani.