Hilari na Tasyani
Hilari na Tasyani (walifariki Aquileia, leo nchini Italia, 284) walikuwa Wakristo ambao waliuawa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Numeriani wa Dola la Roma[1].
Hilari alikuwa askofu wa pili wa Aquileia kuanzia mwaka 276 na Tasyani anasemekana alikuwa shemasi wake.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |