Hirbadaw ni kata ya Wilaya ya Hanang katika Mkoa wa Manyara, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,903 waishio humo.[1]

Wenyeji wa kata hiyo ni Wanyiramba, Wanyaturu, Wairaqw na Wabarbaig.

Kata ina vijiji vinne, yaani: Hirbadaw, Maisaka, Mwanga na Sasumwega na imepakana na Wilaya ya Mkalama (Mkoa wa Singida).

Wakazi wa Hirbadaw hutegemea kilimo na ufugaji. Hujishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi, mtama, maharage, alizeti, vitunguu, ngano n.k.

Kata ya Hirbadaw ina shule moja ya sekondari ya kata ambayo ni Hirbadaw Secondary School (S 1981) na inachukua wanafunzi kutoka shule nne za msingi.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Hanang - Mkoa wa Manyara - Tanzania  

Balang'dalalu | Bassodesh | Bassotu | Dawar | Dirma | Dumbeta | Endagaw | Endasak | Endasiwold | Ganana | Garawja | Gehandu | Gendabi | Getanuwas | Gidahababieg | Gisambalang | Gitting | Hidet | Hirbadaw | Ishponga | Jorodom | Katesh | Laghanga | Lalaji | Masakta | Masqaroda | Measkron | Mogitu | Muldabaw | Nangwa | Simbay | Sirop | Wareta


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hirbadaw kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.