Hispaniola
Hispaniola (kutoka matamshi ya Kilatini ya jina la Kihispania "La Española" = "cha Kihispania") ni kisiwa kikubwa cha pili katika Karibi kikiwa na eneo la km² 74,700.
Iko kati ya Kuba upande wa magharibi na Puerto Rico upande wa mashariki.
Hispaniola huhesabiwa kati ya visiwa vya Antili Kubwa. Ni kile chenye watu wengi zaidi katika Amerika, na cha kumi duniani.
Mashariki mwa kisiwa yalitawaliwa na Hispania kama koloni la Santo Domingo, ilhali Wafaransa walianzisha koloni lao upande wa magharibi wa kisiwa kwa jina la Saint Domingue.
Hivyo leo kisiwani kuna nchi huru mbili: Haiti upande wa magharibi na Jamhuri ya Dominikana upande wa mashariki.
Nchi | Wakazi (2005-07-01 kadirio) |
Eneo (km²) |
Msongamano wa watu(kwa km²) |
---|---|---|---|
Haiti | 9,996,731 | 27,750 | 350.27 |
Jamhuri ya Dominikana | 9,445,281 | 48,730 | 197 |
Kisiwa chote | 19,442,012 | 76,480 | 254.21 |
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Google maps
- Map of the Islands of Hispaniola and Puerto Rico from 1639
- The Kraus Collection of Sir Francis Drake at the Library of Congress contains primary materials on Hispaniola.
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hispaniola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |