Historia ya Ufalme wa Muungano
Historia ya Ufalme wa Muungano inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Ufalme wa Muungano.
Milki kubwa kwenye kisiwa cha Britania ilikuwa Uingereza.
Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Hati ya Muungano (Act of Union) ya mwaka 1536 ilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza.
Hati ya Muungano ya mwaka 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Nchi zote mbili zilikuwa chini ya mfalme mmoja tangu mwaka 1603. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia.
Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).
Baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.
Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.
Mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Northern Ireland zilirudishwa mabunge yao ya pekee.
Uskoti ulikuwa na harakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Muungano lakini katika kura ya watu wa Uskoti ya mwaka 2014 asilimia 55 waliamua kubaki.
Kumbe kura ya wananchi wa Ufalme mzima ya mwaka 2016 iliamua kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ufalme wa Muungano kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |