Ghuba ya Bengali
Ghuba ya Bengali ni hori kubwa ya Bahari Hindi kati ya Bara Hindi, Rasi ya Malay na Sri Lanka yenye umbo la pembetatu. Jina la Bengal limetokana na jimbo la Bengali ya Magharibi katika Uhindi na nchi ya Bangladesh. Bahari ya Andamani inahesabiwa wakati mwingine kuwa sehemu ya ghuba ya Bengal lakini mara nyingi hutazamiwa kama gimba la maji la pekee.
Nchi jirani
haririNchi zinazopakana na ghuba ni Sri Lanka, Uhindi, Bangladesh na Myanmar. Kama Bahari ya Andamani inahesabiwa kuwa sehemu ya ghuba hata nchi za Uthai na Indonesia zinapaswa kutajwa hapa.
Mito inayoishia humo
haririMito mikubwa ya Bara Hindi inayoishia katika Ghuba ya Bengali ni: mto Ganga, mto Meghna, mto Brahmaputra, mto Godavari, mto Krishna na mto Kaveri.
Mto Ayeyarwady wa Myanmar unaishia pia katika ghuba hii.
Bandari
haririBandari muhimu kwenye ghuba ni:
- katika Bangladesh: Chittagong na Mongla
- katika Uhindi: Chennai (zamani Madras), Vishakhapatnam, Kolkata (zamani Calcutta) na Pondicherry