Bahari ya Andamani
Bahari ya Andamani (kwa Kiingereza: Andaman Sea) ni bahari ya pembeni ya Bahari Hindi. Iko kando ya Ghuba ya Bengali.
Mpaka nayo ni safu ya visiwa vya Andamani na Nikobari upande wa magharibi. Upande wa mashariki Bahari ya Andamani inapakana na nchi zifuatazo: Myanmar (au Burma), Uthai na Malaysia. Upande wa kusini kipo kisiwa cha Sumatra (Indonesia).
Eneo lake ni km2 797,000. Urefu kutoka kaskazini hadi kusini ni mnamo kilomita 1,200, upana wake hauzidi km 650. Kina cha wastani ni mita 870, lakini kinafikia hadi mita 4,180. Halijoto ya maji kwenye uso wa bahari hucheza baina ya sentigredi 27.5 hadi 30.
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Andamani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |