Huduma ya Vijana kwa Taifa

Huduma ya vijana kwa taifa

Huduma ya Vijana kwa Taifa (kwa Kiingereza: National Youth Service; kifupi: NYS) ni shirika chini ya Serikali ya Kenya katika Wizara ya Huduma ya Umma, Vijana na Jinsia. Lilianzishwa mwaka 1964 ili kuwafunza vijana mambo muhimu ya kitaifa.

Kabla ya mwisho wa miaka ya 1980, ilikuwa lazima kushiriki katika huduma hiyo kabla ya kujiunga na vyuo vikuu. Leo, makurutu huandikishwa kwa kujitolea. Makurutu hupewa mafunzo msingi ya kijeshi na kuwa na fursa ya kuendelea zaidi mafunzo ya ufundi au kujiunga na Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.

Mwaka 2013, serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilianza mageuzi ya huduma ili kutatua ukosefu wa hali ya juu wa ajira kwa vijana nchini Kenya. Huduma iliyorekebishwa ilizinduliwa mwezi Septemba 2014. Iliruhusu makurutu kutoka vikundi vya jamii ambao waliruhusiwa kuajiriwa na shirika hili bila kupata mafunzo ya kijeshi.

Mwaka 2015 huduma ilihusika katika kashfa iliyokuwa katika Wizara ya Ugatuzi na Mipango. Kashfa hii ilimfanya Katibu wa Wizara, Anne Waiguru, na mkurugenzi mkuu wa NYS, Nelson Githinji kujiuzulu. Richard Ethan Ndubai aliapishwa kama mkurugenzi mkuu mpya mnamo Januari 2016.

Shughuli

hariri

NYS hushiriki katika[1]

Waliomaliza mafunzo ya kijeshi huwa na fursa ya kupata mafunzo ya ufundi katika kilimo na uhandisi.

Marejeo

hariri
  1. "National Service". NYS. 2016-01-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-04. Iliwekwa mnamo 2017-12-04.
  2. Joseph Ndunda. "180, 000 security officers to man Tuesday General Election | The Star, Kenya", The-star.co.ke, 2017-08-04. Retrieved on 2017-12-04. Archived from the original on 2017-08-06.