Trafiki
Trafiki ni jumla ya watumiaji wa njia za usafiri, hasa barabara, kama vile magari, mabasi, malori, waenda kwa miguu na mikokoteni. Ni pia jina la askari maalumu anayesimamia usalama barabarani[1]. Mtandaoni, neno trafiki lina maana ya idadi ya watumiaji wanaotembelea tovuti.
Matumizi
haririNchini Kenya neno "trafiki" hutumika kumaanisha jumla ya watumiaji wa njia ya usafiri. Kwa mfano, Idara ya Trafiki ya polisi, sheria za trafiki na maafisa au polisi wa trafiki[2].
Nchini Tanzania, neno "trafiki" hutumika kama kuwa rejelea askari wa usalama barabarani[3].
Sheria za trafiki
haririSheria za trafiki au pia sheria za barabarani ni sheria na taratibu zinazofuatwa ili kudumisha usalama kwa manufaa ya watumiaji wote wa barabara. Sheria msingi za barabarani zimeelezwa katika mkataba wa kimataifa, Mkataba wa Vienna wa Trafiki Barabarani wa mwaka 1968 ulio chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Kimsingi, mataa ya trafiki yanafaa kuzingatiwa, waenda kwa mguu wanafaa kupatia magari njia isipokuwa katika kivuko cha milia, waenda kwa mguu wanafaa kuwa makini wanapovuka barabara na magari yanafaa kutumia upande wa kuendeshea kulingana na sheria za nchi.
Kila nchi ina sheria msingi za barabarani. Serikali za mashinani kama zile za miji na kaunti zinaweza kuongezea kulingana na mahitaji yake. Sheria ya trafiki ya Kenya (kwa Kiingereza: Traffic Act Ilihifadhiwa 13 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.) ndiyo sheria kuu ya barabarani.
Msongamano wa magari
haririMsongamano wa magari ni hali inayotokea wakati kuna magari mengi barabarani na kufanya mwendo wa magari kuwa wa polepole au kukoma. Majiji makubwa kama vile Nairobi na Dar es Salaam huathirika na hali hiyo hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hii huathiri sana uchumi. Jiji la Dar es Salaam limejaribu kusuluhisha tatizo hili kwa kujenga mfumo wa mabasi ya mwendokasi[4].
Tanbihi
hariri- ↑ "Kamusi ya Oxford". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-12. Iliwekwa mnamo 2018-03-19.
- ↑ "Maafisa wa trafiki kuendesha misako dhidi ya madereva walevi wikendi hii", Milele FM, ilipatikana 19-03-2018
- ↑ "Trafiki hatakiwi kufanya haya kwa dereva", Elizabeth Edward, ilipatikana 19-03-2018
- ↑ "LESSONS FROM DAR ON UNCLOGGING CITY TRAFFIC JAMS – PHOTOS", Nairobi News, ilipatikana 10-03-2018
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Trafiki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |