Kicheche

(Elekezwa kutoka Ictonyx)
Kicheche
Kicheche-nyoka (Poecilogale albinucha)
Kicheche-nyoka (Poecilogale albinucha)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Fischer, 1817
Nusufamilia: Mustelinae (Wanyama wanaofanana na chororo)
Fischer, 1817
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 6:

Vicheche au cheche ni wanyama wa jenasi mbalimbali katika familia Mustelidae. Wanyama hawa ni miongoni mwa wale wanaotoa vundo mbaya kabisa. Wataalamu wengine wanadai kwamba kicheche wa kawaida ananuka vibaya kuliko wanyama wote. Vundo hii inatoka matezi karibu na mkundu kama mnyama akitishwa, na kwa kawaida adui atoroka. Spishi zote zina pua, kidari, tumbo na miguu nyeusi. Zile za Afrika zina milia myeupe na myeusi mgongoni, zile za Amerika zina mgongo kijivu na ile ya Ulaya ina mgongo njano wenye madoa meusi. Vicheche hula wanyama wadogo, ndege na mijusi, wadudu, samaki, amfibia, nyoka na hata matunda na manyasi.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri