Irene Paul
Irene Paul ni mwigizaji wa filamu za Tanzania ambaye anawakilisha vizuri sanaa ya uigizaji Tanzania kwani ameshiriki katika sinema kadhaa za kimataifa.
Irene Paul | |
---|---|
| |
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mwigizaji |
Watoto | Mmoja |
Pamoja na uigizaji, ni mjasiriamali ambaye anatangaza kazi zake na sasa ameanzisha brand yake inayojighulisha na uuzaji wa bidhaa za nywele asilia na mwili inayoitwa 'naturaliSTAR',katika moja ya kitu kilichomsukuma katika hilo ni kumuaminisha mtoto/mwanamke wa kiafrika kwamba anatosha kama alivyo,hili nalo limepelekea yeye kuwaonyesha kwamba uzuri uko wa asili hasa nywele za kiafrika ni sababu tosha ya urembo wako.
Irene ni mke na mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Wendo-Isabel, Irene ni mwanamke anayependa kuficha mambo yake sana na hilo humpelekea kutokuchanganya kazi na maisha yake binafsi. Anaamini kwamba watu au mashabiki wake walimpokea kutokana na kazi afanyazo na sio vinginevyo na ndiyo sababu kubwa ya kutokuwepo kwenye skendo wala sehemu za starehe sana hasa zisizomuingizia pesa.
"Ninatamani mtoto wa kiafrika afikie ndoto zake zote bila kuangalia rangi au nywele yake Bali kile alichonacho ndani yake,ninaamini kila mtu ni nyota inayongara nafasi unayopewa kuonyesha ulichonacho ndio anga....NGARA PASIPO MASHAKA YA ULIVYOUMBWA" anasema Irene.
Sinema alizoshiriki
hariri- 1. Mama Ntilie
- 2. Kichupa
- 3. Nipe nikupe
- 4. Majuto
- 5. Fiona
- 6. Chinga Codineta
- 7. Love & Power
- 8. Kibajaji
- 9. Kalunde
- 10. Fikra Zangu
- 11. Penzi la Giza
- 12. Triple L
- 12. I Hate My Birthday
- 13. Handsome wa Kijiji
- 14. The Shell
- 15. Unpredictable
- 16. Kiumeni[1]
Tuzo
haririMuigizaji bora wa kike 2015 (Tanzania Films Awards).
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Irene Paul kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |