Isaka wa Cordoba
Isaka wa Cordoba (alifariki Cordoba, Hispania, 3 Juni 851) alikuwa mmonaki wa Cordoba aliyeuawa na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu aliungama hadharani imani yake ya Kikristo [1].
Kabla ya kujiunga na monasteri alikuwa na cheo kikubwa ikulu.
Baada ya miaka mitatu, dhuluma ilipoanza, alijitokeza kwa hiari yake mahakamani kujadiliana na hakimu kuhusu ukweli wa dini[2], na kwa ajili hiyo alipewa adhabu ya kifo.
Taarifa zake ziliandikwa na Eulogi wa Kordoba[3] [4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/55660
- ↑ Vida de San Isaac de Córdoba Archived 27 Mei 2021 at the Wayback Machine.
- ↑ Latin writings of Eulogius pdf downloads at documentacatholicaomnia.eu
- ↑ Complete Works of Eulogius of Cordoba English translations of Eulogius' writings.
- ↑ Martyrologium Romanum
Vyanzo
hariri- Tolan, John, Medieval Christian Perceptions of Islam, New York: Routledge, 2000. ISBN|0-8153-1426-4
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |