Jermaniko wa Filadelfia
Jermaniko wa Filadelfia (alifariki Smirna, leo nchini Uturuki, 155) alikuwa kijana Mkristo aliyefia dini yake hiyo wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini, pia kwa sababu ushujaa wake wa kumchochea hayawani aliyetumiwa ulisifiwa katika kitabu "Kifodini cha Polikarpo", askofu wake[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ St. Germanicus Catholic Online
- ↑ Page 653 A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |