John Dalton

Mwanakemia na mwanafizikia wa Uingereza (1766-1844)

John Dalton (6 Septemba 1766-27 Julai 1844) alikuwa mwana kemia na fizikia wa Uingereza (alizaliwa Cumberland).

John Dalton.

Anafahamika sana kwa sababu ya ugunduzi wake wa nadharia ya atomu. Pia alifanya masomo ya kwanza ya upofu wa rangi.

Nadharia ya atomu ya Dalton

hariri

Nadharia ya Dalton ni nadharia ya kisayansi kuhusu atomu. Aliunda nadharia hiyo kuelezea kuhusu vipi elementi zingeungana kwa njia fulani. Wazo la atomu lilikuwa limekwisha kuwako kwa wakati ule lakini lilikuwa halikubaliki kwa upana zaidi. Nadharia ya Dalton ilikuwa imejikita zaidi katika muonekano wa kawaida. Lakini kabla ya hapo ilikuwa imejikita sana katika falsafa.

Nadharia yake ilikuwa ikisema:

  • Kila kitu (maada) imeundwa na atomu
  • Hakuna kinachoweza kuwa kidogo zaidi ya atomu
  • Atomu haiwezi kuundwa ama kuharibiwa
  • Mabadiliko ya kikemikali yanaweza kutokea pale atomu inapo zunguka,kuwekwa au kutolewa kwenye kundi fulani la atomu
  • Atomu za elementi moja zipo sawa kwa sababu zina uzito sawa wa kiatomu

Japokuwa anahusishwa katika nadharia za siku hizi, lakini alikuwa akifanya makosa katika sehemu mbalimbali kwenye nadharia yake. Sasa tunafahamu kwamba atomu inaweza kuundwa au kuharibiwa kwa kazi za nyuklia. Pia tunatambua kuwa atomu inaweza kuwa na uzito tofauti wa kiatomiki, lakini kwa vyovyote ameleta mchango katika ugunduzi wa vitu vingi kuhusu atomu katika sayansi, hasa kemia.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Dalton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.