Jonas Savimbi
Jonas Malheiro Savimbi (3 Agosti 1934 - 22 Februari 2002) alikuwa kiongozi wa vita vya msituni nchini Angola.
Mwaka 1966 alianzisha tapo la UNITA (kwa Kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno. UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana.
UNITA ilianza kama kikundi cha kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya Wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA (kwa Kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho) iliyosaidiwa na Urusi.
Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na kuunda serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Savimbi alipata kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA. Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire), Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua.
Savimbi aliuawa vitani tarehe 22 Februari 2002. Muda mfupi baadaye UNITA na MPLA zilikubaliana kusimamisha mapigano. UNITA ilichukua nafasi ya chama cha upinzani. Hata hivyo taratibu za kidemokrasia zilichelewa hadi chaguzi za miaka 2008 na 2012 na toleo la katiba mpya la mwaka 2010.
Viungo vya nje
hariri- Tamko la Ikulu ya Marekani kuhusu mkutano kati ya rais wa Marekani na Jonas Savimbi, June 30, 1988" Archived 6 Machi 2016 at the Wayback Machine..
- "The Coming Winds of Democracy in Angola" - Hotuba ya Jonas Savimbi nchini Marekani, Oktoba 5, 1989 Archived 1 Januari 2008 at the Wayback Machine.
- Habari ya BBC kuhusu kifo cha Savimbi,
- Tamko la serikali ya Angola kuhusu kifo cha Jonas Savimbi
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jonas Savimbi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |