Jura
Kipindi cha Jura (jurassic) ni kipindi cha pili cha kijiolojia katika enzi ya kimesozo. Ilianza miaka milioni 200 iliyopita, na ilimalizika miaka milioni 145 iliyopita. Kipindi cha Kijura kilitokea baada ya kipindi cha Trias (triassic) na Chaki.
Jina
haririJina linatokana na milima ya Jura (Uswisi) ambako mara ya kwanza matabaka ya miamba ya mashapo yaligunduliwa kama dalili za kipindi maalumu katika historia ya Dunia. Kwa Kiingereza umbo la "Jurassic" ni kawaida.
Tabianchi ya Jura
haririWakati wa Jura, tabianchi ya Dunia ilikuwa na joto na mvua nyingi kuliko leo. Viwango vya dioksidi kabonia hewani na usawa wa bahari pia vilikuwa juu kuliko leo.
Mwanzoni mwa kipindi cha Jura mabara ya Dunia yalikuwa pamoja yakiunda bara kuu la Pangaia lililoanza kuvunjika wakati ule. Juu kabisa ilikuwa inaanza kuvunjika na kuunda chanzo cha Bahari Atlantiki, na kusababisha Bahari nyembamba ya Atlantiki.
Gandunia
haririMwanzoni mwa kipindi cha Jura, bara kuu la Pangaia liligawanyika kwa vipande vya Laurasia upande wa kaskazini na Gondwana upande wa kusini. Mchakato huu uliounda hatimaye mabara ya leo ulichukua muda mrefu sana.
Kwenye mwisho wa Jura, Amerika Kusini ilikuwa imeanza kuachana na Afrika. Upande wa magharibi wa Amerika Kaskazini, safu za milima zilianza kutokea zilizoendelea kuwa Milima ya Rocy Mountains. [1]
Uhai - wanayama
haririUhai duniani uliendelea kufuata mabadiliko yaliyowahi kuanza wakati wa Trias. Jura ilikuwa kipindi cha kwanza cha kustawi kwa dinosauri. Nyayo zao zilipatikana mahali mbalimbali ndani ya miamba ya wakati ule.
Mifupa ya ndege asilia ya archaeopteryx ilipatikana pia katika miamba ya Jura, pamoja na visukuku vya kwanza vya mamalia vinavyopatikana pia ndani ya miamba ya Jura. [2] Mamalia hao walikuwa wadogo tu.
Uhai - mimea
haririKutoka kipindi hicho kuna visukuku vingi vya miti iliyofanana na misonobari. Mimea ya kangaga ilipatikana kwa wingi pia, spishi kadhaa zilikuwa kubwa kama miti. [3]
Marejeo
hariri- ↑ Levin, Harold 2006. The Earth through time. Wiley, Hoboken N.J. Chapters 13 & 14.
- ↑ Benton M. 1990. The reign of the reptiles. Crescent, N.Y.
- ↑ Amos, Jonathan 2019. Mission Jurassic: searching for dinosaur bones. BBC News.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jura kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |