Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Zanzibar
Kanisa kuu la Mt. Yosefu, Zanzibar (kwa Kiingereza: St. Joseph's Cathedral, Zanzibar) ni kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Zanzibar.
Linapatikana mjini Zanzibar na ni kati ya vivutio vya kihistoria vya mji huo. Liko Baghani Area[1], lakini ni vigumu kufikiwa kati ya njia ndogo za Mji Mkongwe[2], ingawa minara yake pacha inaonekana vizuri kwa mbali[3].
Tangu lijengwe limekuwa likitumiwa na jamii ya Wakatoliki mjini Zanzibar ambapo hadi leo Misa kadhaa hufanyika siku za Jumapili, mbali na zile za kila siku, kama ilivyo kawaida hasa ya makanisa makuu.
Historia yake
haririUjenzi uliongozwa na wamisionari Wafaransa kati ya miaka 1893 na 1898 kwa kuiga kanisa kuu la Marseille[3]. Vigae na kioo cha rangi vililetwa kutoka Ufaransa[1].
Ndani kuna michoro kutoka Agano la Kale iliyoharibika kutokana na ukarabati mbovu wa mwaka 2014.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Saint Joseph's Catholic Cathedral
- ↑ "St. Joseph's Cathedral". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-20. Iliwekwa mnamo 2021-03-16.
- ↑ 3.0 3.1 "St. Joseph's Catholic Cathedral". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-12. Iliwekwa mnamo 2021-03-16.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Zanzibar kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |