Kanisa la Biblia Tanzania
Kanisa la Biblia Tanzania (kifupi: KLB) ni kanisa la Uprotestanti lenye shirika zaidi ya 200 hasa kusini mwa Tanzania, katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, lakini pia katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Kilimanjaro. Kanisa la Biblia hufuata mtindo wa Ndugu wa Plymouth, hivyo kila ushirika unajitegemea na kanisa kwa jumla ni ushirikiano wa shirika zake. Limeandikishwa na serikali kwa namba 5881.

Makao makuu yake kwa mara ya kwanza yalikuwa Mbesa (wilaya ya Tunduru). Baadaye yakahamishiwa Tunduru mjini na tangu mwaka 2024 yako mkoa wa Dodoma.
Kanisa hili lilianzishwa na wamisionari kutoka Ujerumani; tangu 1959 linaendelea kushirikiana na CMML (Christian Mission in Many Lands) hata kama utawala wa kanisa umo mikononi mwa Watanzania.
Pamoja na kazi ya kiroho KLB huendesha pia miradi ya kijamii kama vile shule, vyuo, hospitali na kituo cha kutunza watoto yatima.

Kati ya miradi yake ni
- Kituo cha yatima Mbesa
- Chuo cha maarifa ya nyumbani Bethania
- Chuo cha ufundi Nazareth
- Shule ya msingi ya Mkwaju, Mbesa
- Shule ya Sekondari Call and Vision kidato cha kwanza Hadi cha Sita Mtwara
- Hospitali ya misioni Mbesa
- Kituo cha vijana na hosteli Mtwara
- Chuo cha Biblia Nanjoka - Tunduru
- redio ya uinjilisti kwa lugha ya Kiyao
- Kanisa la Biblia Publishers ni idara ya Maandiko ya Kanisa la Biblia Tanzania. Kazi yake ni kutafsiri, kuandaa na kutoa maelezo ya Biblia kwa Kiswahili.
Kuna pia miradi ya kilimo.
KLB inatoa kozi ya Biblia kwa njia ya barua (Emmaus Shule ya Biblia) na kushirikiana na Chuo cha Biblia Berea (Moshi).
Viungo vya nje
hariri- Kanisa la Biblia Publishers Dodoma Ilihifadhiwa 11 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Biblia Tanzania kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |