Wilaya ya Tunduru
Wilaya ya Tunduru ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Ruvuma, nchini Tanzania. Kwa upande wa kusini Tunduru inapakana na nchi ya Msumbiji, upande wa magharibi na wilaya ya Namtumbo, kaskazini na mkoa wa Lindi na upande wa mashariki imepakana na Mkoa wa Mtwara.[1]
Wilaya ya Tunduru ni moja ya wilaya kongwe nchini kwa kuwa ilianzishwa mwaka 1905 wakati wa ukoloni. Serikali ya Ujerumani ilijenga boma katika eneo la Kadewele karibu na lilipo jengo la Mamlaka ya Mapato TRA kwa sasa.
Katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa ni watu 247,976 [2]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 412,054 [3]. Walio wengi ni kabila la Wayao.
Wilaya ina tarafa 7 ambazo ni Mlingoti, Nalasi, Nakapanya, Nampungu, Matemanga, Lukumbule, Namasakata na Mbesa kwa Tunduru mjini.
Wilaya ya Tunduru kuna shule za sekondari na shule za msingi ambazo baadhi ya shule hizo ni Tunduru Sekondari, Mataka, Frank Weston na Masonya.
Pia wilaya hiyo ina Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Nandembo (Nandembo FDC), ambacho kipo katika kijiji cha Nandembo, na Chuo cha Biblia cha Kanisa la Biblia Tanzania huko Nanjoka.
Kilimo
haririKilimo ndio uti wa mgongo wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwani wananchi walio wengi ndani ya wilaya hutegemea kilimo kama chanzo kikuu cha mapato na hufanya kilimo biashara, uhitaji wa huduma na taarifa sahihi za namna bora kuendesha shughuli hii ni muhimu kuzingatiwa.
Shughuli kubwa za kiuchumi zinazofanywa na wananchi wa Wilaya ya Tunduru ni kilimo cha zao la korosho linalolimwa karibu katika maeneo yote ya wilaya, na mazao mengine kama mpunga, mbaazi, choroko, kunde, ufutan a karanga.
Uvuvi
haririPia watu wa Tunduru wanafanya shughuli za ufugaji wa nyuki, kuku, samaki, mbuzi na ng'ombe, na biashara za aina mbalimbali katika mazingira yao. Wilaya hi ina vivutio mbalimbali vya utalii kama mapori ya akiba ya Sasawala na Muhuwesi, Hifadhi ya Taita ya asili ya Mwambesi ambayo pembezoni mwake yapo maporomoko ya Sunda yaliyoko kwenye Mto Ruvuma. [4]
Utalii
haririWilaya ya Tunduru ina vivutio vingi vya utalii na malikale, Misitu ya Asili,Hifadhi ya Taifa ya Selous,Utamaduni na Hifadhi mbalimbali za malikale zinazopatikana katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Tunduru; vivutio hivi vinaweza kuiingizia Wilaya mapato na kuongeza pato la taifa; ndani ya Halmasahuri ya wilaya ya Tunduru kuna malikale ambazo ni kielelezo cha utamaduni wa wakazi wa Tunduru, kama vile malikale ya hifadhi ya Masonya ambayo ni kambi iliyotumiwa na wanaharakati wa Msumbji wakati wa ukombozi kutoka katika utawala wa ukoloni wa Mreno [5].
Marejeo
hariri- ↑ "Mwanzo". tundurudc.go.tz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
- ↑ [1]
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-07-23. Iliwekwa mnamo 2022-07-23.
- ↑ https://tundurudc.go.tz/economic-activity/utamaduni-na-utalii
Kata za Wilaya ya Tunduru - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania | ||
---|---|---|
Chiwana | Jakika | Kalulu | Kidodoma | Ligoma | Ligunga | Lukumbule | Majengo | Majimaji | Marumba | Masonya | Matemanga | Mbati | Mbesa | Mchangani | Mchesi | Mchoteka | Mchuluka | Mindu | Misechela | Mlingoti Magharibi | Mlingoti Mashariki | Mtina | Muhuwesi | Nakapanya | Nakayaya | Nalasi Magharibi | Nalasi Mashariki | Namakambale | Namasakata | Namiungo | Nampungu | Namwinyu | Nandembo | Nanjoka | Ngapa | Sisi Kwa Sisi | Tinginya | Tuwemacho |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Tunduru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |