Kaukazi

(Elekezwa kutoka Kaukasus)

Kaukazi (kwa Kirusi Кавказ Kawkas; kwa Kigeorgia კავკასიონი Kawkasioni) ni eneo la milima kunjamano ambayo ipo baina ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Kaspi linalohesabiwa kuwa mpaka kati ya Asia na Ulaya almaarufu Ulasia.

Milima ya Kaukazi inavyoonekana kutoka angani

Kaukazi iko katika eneo la nchi Armenia, Azerbaijan, Georgia na Urusi. Kilele chenye kimo kikubwa ni mlima Elbrus upande wa Urusi chenye mita 5,642 juu ya UB.

Hata hivyo, mlima unaojulikana hasa ni mlima Ararat unaosemekana ni mahali pa safina ya Nuhu.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.