Kibada (Dar es Salaam)
Kibada ni kata mojawapo ya Wilaya ya Kigamboni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 17109.
Kata ya Kibada | |
Mahali pa Kibada katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Dar es Salaam |
Wilaya | Kigamboni |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 28,188 |
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 28,188 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,305 waishio humo.[2]
Kibada ina jumla ya mitaa sita ambayo ni Kiziza, Nyakwale, Kifurukwe, Uvumba, Sokoni na Kichangani. Upimaji wa viwanja kwa ajili ya makazi, ulihusisha mitaa miwili tu, yaani mtaa wa Kichangani na mtaa wa Kifurukwe.
Zahanati ipo eneo la stendi ya Kibada, karibu na njia panda ya Dar es Salaam Zoo, Kisiwani, Kongowe na Mjimwema. Jirani na zahanati, kuna kituo cha polisi, nyuma yake kuna jengo la parokia ya Kanisa Katoliki.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania | ||
---|---|---|
Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108) |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kibada (Dar es Salaam) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |