Wilaya ya Kigamboni


Kigamboni ni jina la Wilaya mpya kati ya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 17000, pia jina la kata ndani yake iliyo na postikodi 17107.

Wilaya ya Kigamboni
Wilaya ya Kigamboni is located in Tanzania
Wilaya ya Kigamboni
Wilaya ya Kigamboni

Mahali pa Kigamboni katika Tanzania

Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Kigamboni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 317,902
Feri ya Kigamboni mjini Dar es Salaam
Mapumziko Kigamboni ufukoni

Hadi mwaka 2016 Kigamboni ilikuwa jina la kata pekee, na kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 30,496 waishio humo.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa wilaya nzima walihesabiwa 317,902 na wale wa katac 24,810 [2].

Kigamboni ina umbo la rasi kati ya Bahari Hindi na maji ya bandari. Imetengwa na jiji la Dar es Salaam kwa maji ya Kurasini Creek.

Mawasiliano yapo kwa njia ya feri kati ya Kigamboni na Kivukoni upande wa jiji.

Tangu mwaka 2016 kuna Daraja la Julius Nyerere linalounganisha maeneo karibu na Vijibweni upande mmoja na barabara ya Nelson Mandela (zamani Port Access Road) upande wa jiji.

Kuna pia barabara inayozunguka bandari kupitia Kibada hadi kufika Kilwa Road lakini njia hiyo ni ndefu mno: ni kilomita zaidi ya hamsini hadi kitovu cha jiji kwa njia ya nchi kavu.

Pia Kigamboni katika kata ya Vijibweni ndiyo sehemu ambapo kuna yadi nyingi za mafuta: kampuni zinazohifadhi mafuta katika yadi hizo ni: CAMEL OIL, OIL COM, BIG BON na nyinginezo.

Kiasili sehemu hii ilikuwa kijiji cha wavuvi lakini katika miaka ya nyuma watu wa jijini wamejenga nyumba na hoteli za kitalii zimeenea kwenye ufuko wa Bahari Hindi.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania  

Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108)