Kibada (Dar es Salaam)

(Elekezwa kutoka Kibada (Kigamboni))


Kibada ni kata mojawapo ya Wilaya ya Kigamboni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 17109.

Kata ya Kibada
Kata ya Kibada is located in Tanzania
Kata ya Kibada
Kata ya Kibada

Mahali pa Kibada katika Tanzania

Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Kigamboni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 28,188

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 28,188 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,305 waishio humo.[2]

Kibada ina jumla ya mitaa sita ambayo ni Kiziza, Nyakwale, Kifurukwe, Uvumba, Sokoni na Kichangani. Upimaji wa viwanja kwa ajili ya makazi, ulihusisha mitaa miwili tu, yaani mtaa wa Kichangani na mtaa wa Kifurukwe.

Zahanati ipo eneo la stendi ya Kibada, karibu na njia panda ya Dar es Salaam Zoo, Kisiwani, Kongowe na Mjimwema. Jirani na zahanati, kuna kituo cha polisi, nyuma yake kuna jengo la parokia ya Kanisa Katoliki.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
  Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania  

Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108)