Kibosho

Kibosho ni jina la eneo kwenye mitelemko ya mlima Kilimanjaro katika Tanzania. Wakazi wake ni Wachagga. Mwaka 2012 ni sehemu ya kata za Kibosho Kati, Kibosho Magharibi na Kibosho Mashariki katika wilaya ya Moshi Vijijini.

Katika siku za kwanza za ukoloni eneo lake lilikadiriwa kuwa na kilomita za mraba 45 zilizokaliwa na watu wengi kati ya mpaka wa msitu wa mlima Kilimajaro kwa uwiano wa mita 1650 na kutelemka hadi mita 1200 juu ya UB. Mto Karanga unapita katika nchi hii. [1]

Wamangi wa KiboshoEdit

Katika karne ya 18 na 19 na chini ya ukoloni hadi uhuru Kibosho kilikuwa eneo la utemi mdogo wa Kichagga na watawala wake walijulikana kwa cheo cha "Mangi". Kuhusu Wamangi wa kwanza majina yamehifadhiwa lakini tarehe za utawala hazina uhakika. [2]

.... - .... Yansanya [1st ruler]
.... - .... Orio
.... - .... Kimboka
.... - .... Irongo
.... - .... Iweri
takr. 1810 Kirenga
takr. 1850 Kashenge
takr. 1850 - af.1862 Tatua
18.. - 18.. Ngaluma
18.. - 18.. Lokila
18.. - takr. 1872 Mamka (wa kike)
takr. 1872 - 1897 Sina
1897 - 1900 Molelia
1900 - 1911 Sianga
1911 - 1917 Malamya
1917 Barnabas Ngowi (mtendaji)
1917 - 1946 Ngulisho I (+ 1962)
1946 - 1961 Alex Ngulisho II

Mangi Sina alitawala wakati wa kufika kwa wakoloni Wajerumani. Mwaka 1889 alifaulu kumshinda Mangi Rindi wa Moshi lakini kuingilia kwa Wajerumani chini ya Hermann von Wissmann ilikuwa chanzo cha kumaliza mashindano kati ya Wamangi na utawala wa wakoloni katika Uchagga wote.

MarejeoEdit

  1. ling. makala "Kiboscho" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)
  2. orodha ifuatayo ni kutoka http://www.worldstatesmen.org/Tanzania_native.html