Kibungo Juu ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67228.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,304 [1] walioishi humo.

Kata ya Kibungo juu inaundwa na vijiji vitano navyo ni: Kibungo Juu, Lanzi, Nyingwa, Dimilo na Lukenge. Kuna shule za msingi tano, moja kwa kila kijiji.

Wananchi wa kata ya Kibungo ni wakulima wa mazao ya biashara kama vile karafuu, hiriki, tangawizi, bizari, ndizi, lakini wanalima pia mazao ya chakula kama vile mpunga, mahindi, mihogo, magimbi na mengineyo.

Tamaduni za wananchi wa Kibungo Juu hazina tofauti na zile za Waluguru wengine; kwa uchache ni wakarimu na wanaheshimu akina mama; ndiyo maana ukoo unakwenda kwa kufuata mama.

Kiimani wananchi wa kata hiyo wamegawanyika katika dini kubwa mbili: Waislamu na Wakristo.

Marejeo hariri

  1. Sensa ya 2012, Morogoro - Morogoro DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-03.
  Kata za Wilaya ya Morogoro Vijijini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Bungu | Bwakila Chini | Bwakila Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibuko | Kibungo Juu | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde (Morogoro) | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tomondo | Tununguo


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kibungo Juu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.