Kipiri

(Elekezwa kutoka Kifutu)
Kipiri
Kipiri usiku Causus rhombeatus
Kipiri usiku
Causus rhombeatus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Viperidae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Ngazi za chini

Jenasi 34:

Vipiri au vifutu ni spishi za nyoka wenye sumu katika familia Viperidae. Spishi nyingine huitwa bafe au moma pia.

Nyoka hawa sio warefu sana lakini wanene kwa kulinganisha na nyoka wengine na wana kichwa kipana kwa umbo wa pembetatu na mkia mfupi. Kwa kawaida magamba yao yana miinuko ambayo inaweza kuwa kama miiba. Miboni ya macho ni kama chanjo za wima ikiwa imefungwa kwa kiasi.

Waking'ata vipiri huingiza sumu katika mwili kupitia chonge mbili zenye mifereji. Mdomo ukiwa umefungwa chonge hizi zinalala kutegemea dari lake. Lakini iwapo kipiri akifungua mdomo chonge huduru mbele ili kudunga. Misuli inayofunga mdomo inakamua pia sumu kutoka tezi.

Vipiri sio wepesi sana na kwa hivyo wako hatari. Kwa sababu wana rangi za kamafleji hukaa bila kusogea hata kama adui anakaribia. Mtu anaweza kumkanyaga kipiri bila kumwona kisha kuumwa na kudungwa sumu. Lakini wakati mwingine kipiri anauma bila kuingiza sumu.

Sumu ya vipiri ina vimeng'enya vingi vinavyomeng'enya proteini (proteasi). Mchakato huu unasababisha maumivu makali, uvimbe na kuoza kwa tishu. Hata akipona mwathirika atakaa na kovu.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri

Spishi za sehemu nyingine za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kipiri kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.