Kiiraqw
Kiiraqw ni mojawapo kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiiraqw iko katika kundi la lugha za Kikushi.
Inatumika na kuzungumzwa hasa na kabila la Wairaqw kaskazini mwa Tanzania kutokana na kuwepo kwao katika mkoa wa Manyara na mkoa wa Arusha kama wenyeji wa karne nyingi.
Baadhi ya watu husema Kiiraqw ni sawa na "Kimbulu", kumbe siyo. Hakuna lugha inayoitwa Kimbulu. Mbulu ni jina la wilaya ambayo ina idadi kubwa ya Wairaqw kuliko eneo lingine lolote nchini Tanzania. Lakini ikumbukwe kuwa Mbulu si eneo pekee wanakopatikana Wairaqw, kitu ambacho kingesababisha watu wengine kuita lugha ya Kiiraqw kuwa Kimbulu.
Mwaka 2001 idadi ya wasemaji wa Kiiraqw ilihesabiwa kuwa watu 462,000. Kwa sasa wanakadiriwa kuwa milioni 1 hivi.
Kiiraqw, kama moja ya lugha zinazozungumzwa nchini Tanzania, ni lugha ambayo haina ufanano wa aina yoyote na lugha za Kibantu kama Kiswahili, Kisukuma, Kingoni, Kinyakyusa n.k.
Vitenzi katika lugha za Kibantu vimeishia na irabu, jambo ambalo ni tofauti kabisa katika lughà ya Kiiraqw ambapo vitenzi vyake vyote vinaishia na konsonanti. Mifano: neno "nenda" Kwa Kiiraqw ni "tlaw", "kula" ni "ãyiim", Lima ni "dosl"
Pamoja na utangulizi huo, utafiti wa kina unapaswa kufanyika ili kuielewa vizuri lugha hiyo na kuja na matokeo makubwa zaidi
Marejeo
hariri- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346
Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:
- Maghway, Josephat B. 1995. Annotated Iraqw lexicon. (African language study series, vol 2.) Tokyo: Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and Africa (ILCAA), Tokyo University of Foreign Studies. Kurasa 210.
- Mous, Maarten. 1993. A grammar of Iraqw. (Cushitic language studies/ Kuschitische Sprachstudien, vol 9.) Hamburg: Helmut Buske Verlag. Kurasa xvi, 361. [ISBN 3-87548-057-0]
- Desdery Sulle; (2013) Short research on Kiiraq; as a Cushitic Language speaker.
- Desdery Sulle; (2014). An investigation on verb derivations in Iraqw language (In relation to increase and decrease the number of arguments). Songea. St. Augustine university of Tanzania Library
Viungo vya nje
hariri- Lugha ya Kiiraqw kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kiiraqw Archived 23 Septemba 2015 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kiiraqw katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/irk
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html Archived 4 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiiraqw kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |