Kikilo ni kata ya Wilaya ya Kondoa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41711[1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 9,620 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9318 [3] waishio humo.

Makao makuu ya Kata yapo katika Kijiji cha Kikilo.

Huduma za jamii hariri

Baadhi ya vijiji vya kata ya Kikilo vyenye shule ya msingi ni: Kikilo yenyewe, Berabera, Kwahengwa na Ororimo.

Kata ya Kikilo ina zahanati moja iliyojengwa katika kijiji cha Kwahengwa. Zahanati hiyo ilijengwa kwa nguvu za wananchi na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mwaka 2017 wakati huo Mkurugenzi wa Wilaya akiwa Mwalimu Falesy Mohamed Kibassa.

Kata ya Kikilo inaunganishwa na kata za Bereko, Salanka na Thawi kwa barabara ya vumbi.

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08. 
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. "Sensa ya 2012, Dodoma - Kondoa DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-18. 
  Kata za Wilaya ya Kondoa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania  

Bereko * Bumbuta * Busi * Changaa * Haubi * Hondomairo * Itaswi * Itololo * Kalamba * Keikei * Kikilo * Kikore * Kinyasi * Kisese * Kwadelo * Masange * Mnenia * Pahi * Salanka * Soera * Thawi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kikilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.