Kisiwa cha Bouvet (kilijulikana kihistoria pia kama Liverpool Island au Lindsay Island) ni kisiwa kisicho na wakazi kusini mwa Bahari Atlantiki takriban kilomita 2500 kusini-magharibi ya Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini).

Kisiwa cha Bouvet

Ni eneo lililopo chini ya Norwei lakini si sehemu ya Norwei yenyewe. Si chini ya mkataba wa Antaktiki inayosema ya kwamba sehemu za Antaktiki yenyewe haziwezi kutawaliwa na nchi yoyote kwa sababu iko bado mbali kidogo. Bouvet inasemekana ni kisiwa ambacho ni mali kabisa na makazi ya watu wowote.

Bouvet ina urefu wa kilomita 9 na upana wa km 7.5, eneo lake huwa na km² 49.

Sehemu ya juu ni mlima wa Olavtoppen wenye kimo cha mita 790 juu ya UB.

Asili ya kisiwa ni volkeno na asilimia 90 za uso wake hufunikwa kwa barafuto kubwa. Hali ya hewa ni baridi sana. Halijoto ya wastani ni +1°C wakati wa miezi ya joto na -3 °C wakati wa baridi.

Viumbehai pekee vilivyopo kisiwani ni ndege na sili.

Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Bouvet kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.