Kisiwa cha Mainland

Mainland ndicho kisiwa kikuu cha funguvisiwa ya Shetland, upande wa kaskazini ya Uskoti (Scotland). Inahesabiwa kuwa sehemu ya Uskoti.

Ramani ya Shetland
Mahali pa Shetland kati ya Uskoti na Norwei

Visiwa vya Shetland viko baharini kati ya Visiwa vya Faroe na Visiwa vya Orkney. Funguvisiwa hii iko mpakani kati ya Bahari Atlantiki upande wa magharibi na Bahari ya Kaskazini upande wa mashariki.

Kwa jumla kuna visiwa 100 na kati yake 16 vinakaliwa na watu 23,510[1]. Eneo lote ni km² 1,426 na theluthi mbili zake ni eneo la kisiwa cha Mainland. Makao makuu ya utawala na mji mkubwa ni Lerwick.

Tabianchi ni nusu aktiki na si baridi sana kutokana na athira ya mkondo wa ghuba.

Uchumi hariri

Uchumi wa visiwa unategemea kilimo na hasa ufugaji wa kondoo.

Mwaka 1969 mafuta ya petroli yaligunduliwa yakawa chanzo kipya cha mapato.

Marejeo hariri