Visiwa vya Shetland

Ramani ya Shetland
Mahali pa Shetland kati ya Uskoti na Norwei

Shetland (au Visiwa vya Shetland) ni funguvisiwa upande wa kaskazini ya Uskoti (Scotland). Inahesabiwa kuwa sehemu ya Uskoti.

Visiwa vya Shetland viko baharini kati ya Visiwa vya Faroe na Visiwa vya Orkney. Kwa jumla kuna visiwa 100 na kati yake 16 vinakaliwa na watu 23,510[1].

Funguvisiwa hii iko mpakani kati ya Bahari Atlantiki upande wa magharibi na Bahari ya Kaskazini upande wa mashariki.

EneoEdit

Visiwa vikubwa zaidi huitwa Mainland, Yell, Unst, Fetlar, Whalsay na Bressay. Tabianchi ni nusu aktiki na si baridi sana kutokana na athira ya mkondo wa ghuba.

Eneo la nchi kavu ni km² 1,426 na theluthi mbili zake ni eneo la kisiwa cha Mainland. Makao makuu ya utawala na mji mkubwa ni Lerwick. Mji wa pili inaitwa Scalloway na hii ni pia kitovu cha kihistoria.

Mwinuko wa juu ni kilima cha Ronas Hill chenye kimo cha mita 449 juu ya usawa wa bahari.

UchumiEdit

Uchumi wa visiwa unategemea kilimo na hasa ufugaji wa kondoo.

Mwaka 1969 mafuta ya petroli yaligunduliwa yakawa chanzo kipya cha mapato.

MarejeoEdit