Visiwa vya Faroe
Visiwa vya Faroe (kwa Kifaroe: Føroyar - "Visiwa vya kondoo") ni funguvisiwa ya Atlantiki ya Kaskazini kati ya Iceland, Uskoti na Norwei.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Tú alfagra land mítt "We nchi yangu nzuri" | |||||
Mji mkuu | Tórshavn | ||||
Mji mkubwa nchini | Torshavn | ||||
Lugha rasmi | Kifaroe, Kidenmark | ||||
Serikali | demokrasia, ufalme wa kikatiba Mfalme Frederik X wa Denmark Aksel V. Johannesen | ||||
Jimbo la nje la Denmark Madaraka ya kujitawala |
1948 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,399 km² (ya 180) 0.5 | ||||
Idadi ya watu - Desemba 2016 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
49,188 (ya 206) 48,346 35.2/km² (ya 169) | ||||
Fedha | Krona ya Faroe2 (DKK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC) EST (UTC+1) | ||||
Intaneti TLD | .fo | ||||
Kodi ya simu | +298
- |
Historia
Wakazi wa kwanza walikuwa wamonaki kutoka Ireland.
Kati ya miaka 1035 na 1814 visiwa vilikuwa chini ya Norwei. Ndipo vilipotolewa kwa Denmark.
Kufikia mwanzo wa mwaka 1540 wakazi walikuwa wamejiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kuwa Walutheri.
Kuanzia mwaka 1948 ni jimbo la nje la ufalme wa Denmark lenye madaraka ya pekee ya kujitawala. Visiwa vinaendesha shughuli zao isipokuwa siasa ya nje, jeshi na mambo ya mahakama ni chini ya serikali kuu. Hali ya kisiasa ndani ya Denmark inalingana na Greenland ambayo pia ni jimbo la nje la Denmark linalojitawala kwa kiwango kikubwa.
Visiwa vya Faroe viliamua kutoingia katika Umoja wa Ulaya pamoja na Denmark. Kumbe vimeunda umoja wa forodha na Iceland.
Watu
Wakazi wengi wana asili ya Skandinavia upande wa baba (87%) na ya Wakelti upande wa mama (84%).
Lugha rasmi ni Kifaroe, lugha ya Kigermanik ya Kaskazini karibu na Kiiceland.
Hadi leo 84.1% za wakazi ni Walutheri na madhehebu yao ndiyo dini rasmi.
Uchumi
Viungo vya nje
- Official site Ilihifadhiwa 4 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- Official tourist site
- Flick photo set
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Faroe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |