Kitajiki
Kitajiki (тоҷикӣ / تاجیکی / tamka "tojiki" au забони тоҷикӣ / زبان تاجکی / tamka "zabone tojiki") ni lugha rasmi nchini Tajikistan katika Asia ya Kati. Kuna pia wasemaji wa Kitajiki katika Urusi na katika Uzbekistan.
Kitajiki kinatajwa mara nyingi kama lahaja ya Kiajemi. Wasemaji wa Kitajiki wanaelewana bila matatizo na wasemaji wa Kiajemi nchini Uajemi au wasemaji wa Kidari nchini Afghanistan.
Kama Kiajemi ni mojawapo ya lugha za Kiirani kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Lugha huandikwa katika Tajikistan kwa herufi za Kisirili kama Kirusi. Hadi miaka ya 1920 iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.